STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amefunguka kuwa albamu yake mpya ya Money Mondays ambayo bado ipo katika matayarisho ikikamilika itauzwa mtandaoni na anaamini itavunja rekodi ya mauzo.
Akichonga na Over Ze Weekend, Vee Money ambaye ameorodheshwa kwa sasa kwenye Tuzo za NEA (Nigeria Entertainment Awards) na AEA USA (African Entertainment Awards USA) ambazo zote zinatolewa mwaka huu aliongeza kuwa katika albamu hiyo itakuwa na mastaa wa ndani na nje kibao (huku akificha majina yao kwa sasa).
“Nimejipanga vizuri kuisambaza mtandaoni na hata kopi za CD kwani nina timu nzuri nitakayofanyanayo kazi pindi albamu ikitoka,” alisema