MSANII kutoka Bongo Muvi, Ester Kiama amesema anajutia kujiingiza katika fani hiyo aliyoitamani muda mrefu baada ya kuona soko limeingia ‘mdudu’ mbaya bora na kwamba bora angeendelea na biashara yake ya upambaji.
Akizungumza na Amani juzikati, Ester alisema zamani alikuwa na shauku ya kutimiza ndoto yake ya kuwa muigizaji mkubwa, lakini alipoanza kujulikana, soko la filamu limekuwa gumu, haziuziki na hata msanii akipeleka kazi yake kwa wasambazaji, malipo yake huchukua mwaka mzima.
“Najuta bora hata ningeendelea na kazi yangu ya saluni na upambaji niliyokuwa nikiifanya awali kuliko kujiingiza huku, soko hakuna. Unacheza filamu unaiweka ndani tu utaipeleka wapi sasa, wanunuaji hawapo, inabidi wadau wafanye kitu kurejesha soko,” alisema Ester.
