×

Kumbe Joh bonge la dairekta

Joh-makini.jpgSTAA wa Hip Hop Bongo, John Simon Mseke ‘Joh Makini’ ameonesha kuwa anaweza kazi ya udairekta baada ya kufungukia ngoma yake mpya ya Perfect Combo kuwa idea ya kutengeneza video (mswada/script) aliitoa yeye.

Akichonga na mtandsao wa Global, Joh Makini ambaye amefanya ngoma hiyo kwa kushirikiana na staa kutoka Nigeria, Chidinma alisema kuwa alianza kuandika idea ya video hiyo itakuwaje na kisha akampatia Dairekta Justin Campos.

“Asilimia kubwa ya video itakuwaje niliitoa mimi nikampatia Justin naye akaongezea vitu vichache ndiyo video ikawa kama inavyoonekana,” alisema Joh.

Leave a Comment