Mwanamuziki Brandy Rayana Norwood ‘Brandy’ ameulalamikia mkataba aliosainishwa na Kampuni ya Chameleon Entertainment akiuita kuwa ni wa kitumwa na yuko kwenye harakati za kuuvunja.
Brandy alisaini mkataba huo tangu mwaka 2011 na aliahidiwa mambo kibao ikiwemo kupewa pesa za kuandaa albamu zake lakini tangu kipindi hicho mambo yamekuwa yakienda ndivyo sivyo.
Alisema kuwa, kampuni hiyo inachofanya zaidi ni kumsimamia yeye kuhakikisha anarekodi nyimbo tu kitu ambacho kinadidimiza fani na maendeleo yake kwa ujumla.
Brandy amefungua kesi huko Los Angeles tangu Machi, 2016 akiidai kampuni hiyo fidia ya kumlostisha sambamba na malipo yake yote yaliyokuwa kwenye mkataba huo.