×

Ferooz awapotezea mademu mastaa

????????????????????????????????????Na Gabriel Ng’osha

Kumbe eeh! Msanii wa ‘long time kitambo’ Ferooz Mrisho amefunguka kuwa hawezi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na demu staa kwa kuwa anajua jinsi walivyo pasua kichwa.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi kwa sasa, msanii huyo alisema kuwa kutokana na jinsi anavyoona wanaume walio na mastaa wanavyohenyeka, yeye hawezi kuingia huko na badala yake amejituliza na mpenzi wake ambaye wala siyo staa.

“Mchumba wangu ni mtu wa kawaida sana, nawaogopa sana mastaa maana ni pasua kichwa kinoma. Najua watu wanataka kumjua niliyenaye, nitafanya hivyo muda ukiwadia,” alisema Ferooz.

Leave a Comment