
NEW YORK, Marekani
WAKATI maandalizi ya kuelekea Michezo ya Olimpiki yakiendelea, tetesi zilizokuwa zikisambaa ni kuwa mkongwe wa mchezo wa kikapu katika Ligi ya NBA, Kobe Bryant atakuwa mmoja wa wachezaji watakaojiunga katika timu ya taifa ya kikapu itakayoshiriki kwenye michezo hiyo.
Kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Mike Krzyzewski amekanusha tetesi hizo kwa kusema hazina ukweli.
“Tulizungumza naye juu ya hilo akasema asanteni lakini hapana,” alisema Krzyzewski ambaye alisoma pamoja na Kobe enzi za ngazi ya chuo.
Bryant aliyekuwa akiichezea LA Lakers alistaafu mwishoni mwa msimu uliopita.