×

Mama Kubwa: Figa Yangu Imenipa Ustaa Wa Fasta

Ismail-mariamNa Imelda Mtema

MSANII nyota wa tamthiliya ya Mama Kubwa inayorushwa hewani kupitia Televisheni ya ITV, Miriam Ismail amesema kuwa, figa yake imemfanya apate ustaa wa fasta na kuwa kipenzi cha watu.

Miriam ambaye hufahamika zaidi kwa jina la Mama Kubwa kutokana na kuwa mrefu na figa ya kufungashia alisema kuwa, alishacheza filamu nyingi huko nyuma lakini ‘hakushaini’ kama ilivyo sasa hivyo anajivunia mwili wake.

“Sasa hapa lazima niupongeze mwili wangu, umenifanya nipate ustaa wa fasta kwa kweli na hii yote ni kutokana na kuuvaa uhusika, ubabe kwa sana, nadhani nisingekuwa na mwili huu wala nisingefiti uhusika niliopewa,” alisema Miriam.

Leave a Comment