×

Trafiki Aliyeuawa Aagwa, Sirro Aahidi Kuwadaka Wauaji

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (2)
Jeneza la marehemu Sajent Alex Njau aliyeuawa usiku wa Ijumaa wiki iliyopita kwa kupigwa risasi.

ASKARI wa usalama barabarani Sajent Alex Njau aliyeuawa usiku wa Ijumaa wiki iliyopita kwa kupigwa risasi mbili kifuani na watu ambao hawajajulikana wakati akiwa kazini, mwili wake umeagwa leo nyumbani kwake maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam na kuanza safari ya kuelekea mkoani kwao Moshi, Mamba-Marangu kwa mazishi.

Katika tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu, Simon Sirro, amesema jeshi litapambana kwa hali na mali kuhakikisha waliohusika na tukio hilo wanachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Nataka niiambie familia ya marehemu kwamba msiba huu umetusikitisha sana na niwaahidi kwamba tutafanya juu chini kuhakikisha wahusika wote waliohusika wanapatikana na wanashughulikiwa ipasavyo kisheria. Lazima wahusika tuwapate wakiwa hai au wamekufa, hata kama aliyehusika yupo ndani ya familia tutamgonga tu,” alisema.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (1)
Ndugu wa marehemu akibebwa baada ya kupoteza fahamu.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (3)
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kinondoni, Awadhi J. Haji, akitoa neno.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (4)
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Simon Sirro akizungumza machache msibani.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (5)
Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azan, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni akieleza machache msibani hapo.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (6)
…Akitoa salamu za mwisho.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (7)

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Christopher Fuime (wa pili kushoto) akiaga mwili wa marehemu.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (8)
Baadhi ya matrafiki wakiaga wakitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (9)
Baadhi ya polisi wakimuaga marehemu.

TRAFIKI ALIYEPIGWA RISASI AAGWA (10)

Jeneza likipakizwa garini tayari kwa safari ya kwenda Moshi.

Na Mayasa Mariwata/GPL

Leave a Comment