Na Leonard Msigwa/GPL
MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic jana kwa mara ya kwanza ameshiriki kufanya mazoezi na wenzake tangu ajiunge na timu hiyo kwenye uwanja wa mazoezi wa Carrington.
Alijiunga na wenzake baada ya kumaliza likizo yake ya mapumziko aliyopewa na uongozi wa timu hiyo baada ya kujiunga na timu hiyo.
Alikuwa akicheka na kutaniana kwa muda mwingi na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney, Phil Jones pamoja na mchezaji mwingine mgeni Eric Bailly.
Anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha timu yake kitakachopambana kwenye mchezo wa kirafiki na timu ya Galatasaray kwenye uwanja wa Gothenburg, uliopo nchini kwake Sweden.




