×

Mtoto Wa Kofi Olomide Akimbiza Kwa Fashion

10654846_473789932804417_406382368_n   Mwanamitindo anayechipukia, Didi Olomide akiwa na baba yake Koffi Olomide.

PARIS, Ufaransa

HUKU baba yake, Koffi Olomide akiachiwa kwa dhamana baada ya kutakiwa kufungwa miezi 18 kwa kumpiga mnenguaji wake

Pame mwanamitindo anayechipukia, Didi Olomide ameanza kukimbiza katika fani ya mitindo nchini Ufaransa hali inayomfanya kila mtu kumtabiria mazuri huko mbeleni.

12393606_104672193248588_570569374_n

Didi Olomide akiwa katika pozi.

Koffi Olomide raia wa DR Congo, juzi kati alitimuliwa nchini Kenya alikokwenda kwenye shoo kutokana na kusambaa kwa video iliyomuonyesha akimpiga teke dansa wake, hivyo kutiwa jela kwa muda wa miezi 18.

13734468_1821981128030355_699529984_n

Akisikiliza musiki.

Didi, 16, ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali kwa kuwa na umbo kali kiasi kwamba jarida ‘bab kubwa’ la Vogue liliamua kuzitumia picha zake na kuweka maneno ya kumsifia kutokana na muonekano wake wa umbo, mavazi na nywele.

13671882_617747395046354_610109745_n

Wakifanya yao na baba yake.

Watu wengi wamekuwa wakimsifia katika mitandao ya kijamii hasa Instagram na kumtabiria kwamba atakuwa tishio siku za usoni kwani kitendo cha kusifiwa na jarida hilo kimemfanya kukubalika huku yeye mwenyewe akiwa na ndoto za kuwa mmoja wa wanamitindo wanaosimamiwa na mwanamitindo Jean Paul Gaultier.

 

 

Leave a Comment