×

Mtoto Aliyeteswa, Apata Hifadhi Serikalini

mtoto ateswa picha na global publishers (5) Mtoto Miriam akionesha majeraha.

Na Issa Mnally, UWAZI

DAR ES SALAAM: Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kinondoni, imemhifadhi Miriam (10) baada ya kuona akinyanyaswa kupita kiasi na mama yake (jina linahifadhiwa), ambaye ni mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam.

mtoto ateswa picha na global publishers (4)Mjumbe wa Shina Na. 063 Mavurunza A, Mtaa wa Kwakichwa, Janet Moshi amethibitisha kuchukuliwa kwa mtoto huyo, baada ya wazazi wake kukimbia nyumba yao na kupotelea kusikojulikana baada ya kuanza kutafutwa na polisi.

mtotooooMtoto Miriam baada ya kupata hifadhi.

Mjumbe huyo alidai kuwa kutokana na unyanyasaji ambao amekuwa akifanyiwa, hata mahudhurio ya binti huyo shuleni yamekuwa hayaridhishi. Baada ya kumuokoa kutoka kwenye mikono ya wazazi hao, majirani pamoja na mjumbe huyo walimpeleka polisi.

mtoto ateswa picha na global publishers (1)Mmoja wa majirani wa binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Donata, aliliambia gazeti hili kuwa mtoto huyo hivi sasa yupo katika mikono salama ya serikali  akilelewa na ustawi wa jamii na anaendelea vizuri.

“Yule mama na mumewe wametoroka, wanatafutwa ili washtakiwe, hatujui wamekimbilia wapi,” alisema mama huyo na kulimwagia sifa Gazeti la Uwazi kuwa ndilo lililofanikisha mtoto huyo kuchukuliwa na serikali.

 Binti miaka 8 afanyiwa ukatili wa kutisha!

Leave a Comment