×

Kisa skendo… Duma hafikirii kuoa kwa sasa

Daudi Michael ‘Duma’Stori: BMM, Jumamosi

MUIGIZAJI aliyekuza jina zaidi kupitia Tamthiliya ya Siri ya Mtungi, Daudi Michael ‘Duma’ amesema kuwa kwa sasa hafikirii suala la kuoa kwa sababu ya changamoto hasa za kimapenzi anazokutana nazo kwenye uigizaji.

Akipiga stori kiaina na safu hii ya burudani, Duma aliongeza kuwa changamoto hizo anafahamu zinamfanya mara kwa mara kuzinguana na wanawake anaoanzisha nao uhusiano kiasi kwamba kwa sasa hana mpenzi na wala hafikirii kabisa kuoa.

“Niko singo kwa sasa, nina watoto wawili lakini sifikirii kabisa kuoa, ninachofikiria ni kazi na nguvu zaidi nimewekeza kwenye filamu yangu hii mpya niliyocheza na mastaa kibao akiwemo Riama, Dude na Mboto,” alisema Duma.

Leave a Comment