
KAMPUNI ya Multchoice Tanzania, juzi ilizindua rasmi msimu wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ ambayo inatarajiwa kuanza rasmi kesho Jumamosi.
Wakati wa uzinduzi huo kupitia DStv, Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania, Maharage Chande, alisema mechi 300 kati ya 380 zitaonyeshwa ‘live’.
Maharage amesema pamoja na kuongeza mechi za live, sasa hadi wenye king’amuzi wanaolipia shilingi 23,500 nao wataona live mechi 100 za ligi hiyo. “Hii ni asilimia 80 ya mechi za Premier League ambacho ni kitu kikubwa. Hakuna king’amuzi kingine kitaonyesha mechi nyingi live kama chetu.
“Pia tutaonyesha mechi nyingine za FA Cup, Capital ONE Cup, Spanish Super Cup, Copa Del Rey Final na German Cup,” alisema Maharage.