Wizkid akipiga shoo.
Shilole na Man Fongo wakipagawisha.
Stori: Iddy Mumba
STAA anayefanya kweli kimuziki Afrika kutoka Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’ amewapa darasa wasanii wa Kibongo kutokana na makamuziki aliyoyafanya kwenye ufunguzi wa Tamasha la Fiesta lililofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na mamia ya wapenda burudani wa jiji hilo.
Kabla ya kuanza kwa tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Imo, Wiz aliwapa elimu wasanii juu ya kila mmoja kufanya kazi kwa bidii bila kukopi kile anachokifanya mwingine hata kama ni msanii wa nje, lakini kwenye shoo alionesha uwezo mkubwa wa kulimiliki jukwaa pamoja na kucheza na mashabiki baadhi ya nyimbo zake zikiwemo Ojuelegba na Final jambo ambalo wasanii wengi wa Kibongo hawawezi kulifanya.
Hata hivyo, katika tamasha hilo wasanii mbalimbali wakiwemo Chege, Ben Pol, Maua Sama, Navy Kenzo, Shilole, Man Fongo, Fid Q walipata nafasi ya kukamua ambapo baada ya Mwanza timu nzima ya Fiesta inaelekea pande za Kahama mkoani Shinyanga.



