×

Diamond Ashindwa Kujizuia, Awalipua Forbes Kuhusu Utajiri Wake -Video

Staa wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul, maarufu Diamond Platnumz leo Mei 18, 2021 kupitia ukurasa wake wa Instagram amewachana Forbes kumfuatilia vizuri utajiri wake kabla hawajamuweka kwenye orodha ya kipumbavu ya wasanii matajiri Afrika.

 
Diamond ameandika “FORBES: Next time google me to know what am really worth of, before putting me on your Stupid Richest African Musicians List!!!”(Forbes, wakati mwingine mnifuatilie vizuri (google) kujua utajiri wangu kabla ya kuniweka kwenye orodha ya kipumbavu ya wasanii matajri zaidi Afrika”).
 
Hatua hii imekuja baada ya tovuti mbalimbali kuandika kuwa Diamond Platnumz ametajwa na jarida la Forbes kama msanii namba 28 tajiri zaidi barani Afrika akiwa anamiliki utajiri wa dola za Kimarekani Milioni 5 jambo ambalo mashabiki wengi wa Diamond walilipinga kutokana na namba hizo kuwa ndogo ukilinganisha na thamani na uwekezaji alioufanya msanii huyo. #globalpublishersupdaes @forbesafrica

Leave a Comment