KOCHA Mkuu mpya wa timu ya Taifa ya Ubelgiji, Mhispania Roberto Martinez amemteua straika wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa kuwa Kocha Msaidizi wake.
Henry anachukua nafasi ya juu ya ukocha tangu alipotimuliwa na Kocha wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger alikokuwa akifundisha timu ya vijana chini ya miaka 18 kwa Washika Bunduki hao (The Gunners) kabla ya kutimuliwa na Wenger kutokana kuchambua klabu yake hiyo kwenye Luninga ya Sky Sport.
Henry ataruhusiwa kuendelea na uchambuzi kwenye Luniga ya Sky huku akifundisha timu hiyo ya Ubelgiji.
Hiki ndicho kikosi atakachokifundisha Hnery, wamo akina Eden Hazard, Marouane Fellaini na Kevin De Bruyne.

