
KLABU ya Arsenal iko tayari kumtoa kwa mkopo kiungo wake, Jack Wilshere ili kumpa fursa ya kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Uingereza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, msimu uliopita alishindwa kuitumikia vyema klabu yake kutokana na jeraha la mguu lililopelekea kucheza mechi tatu pekee.
Aliichezea Uingereza mechi sita pekee msimu uliopita, zikiwemo mechi tatu katika mashindano ya Euro 2016, lakini hakuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha mkufunzi Sam Allardyce wiki hii.
Arsenal ililipa pauni milioni 35 kumnunua mchezaji wa Switzerland Granit Xhaka msimu huu ambaye anaongeza ushindani klabuni hapo na kumfanya Wilshere akose nafasi ya kudumu klabuni hapo.
