×

‘Uwazi’ Lachangamkiwa na Wasomaji Mabwepande

SAMSUNG CAMERA PICTURES
Msomaji wa gazeti la Uwazi aliyejitambulisha kwa jina la Ibrahim akilisoma gazeti hilo.   Kushoto kwake ni muuzaji wa gazeti hilo Mwamvita Rashid, akimuuzia kwa mteja mwingine.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
’Mr. Uwazi’ akisoma gazeti hilo na msomaji ambaye ni mkazi wa Mabwepande.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Muuzaji wa Uwazi, Mwamvita Rashid, akisoma gazeti hilo na msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Mlindi.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Msomaji wa Uwazi aliyejitabulisha kwa jina la Mndolwa Juma akilisoma gazeti hilo eneo la Mabwepande.

3.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Jimmy Haroub, akisoma gazeti hilo na mdau wake aliyejitambulisha kwa jina la Sophia.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Mwanadada aliyejitambulisha kwa jina la Rehema akisoma Uwazi.

WASOMAJI wa Gazeti la Uwazi, leo walilichangamkia kwa bashasha kubwa katika mitaa ya Mabwepande na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam wakisema wanalikubali kwa habari zake za kijamii na za uchunguzi.

Timu ya gazeti hilo ilitinga eneo hilo na kuzunguka sehemu mbalimbali ambapo wadau kibao walionekana wakiwa wamelinunua na wengine kusogea karibu na gari la matangazo lililokuwa likipita maeneo hayo na kulinunua na kupata zawadi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwa wateja.

Walisema kinachowavutia zaidi ni habari za kijamii na jinsi linavyochimbua matukio mbalimbali ya kila yanayotokea katika jamii na wao kubahatika kuyasoma ndani ya gazeti hilo.

“Kwa kweli Uwazi ndiyo gazeti bora zaidi  Tanzania, habari zake na makala zinanifanya nisiache kulinunua kwani ndilo linaloandika habari za uchunguzi kwa undani,” alisema msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Mndolwa Juma.

Pia mhariri wa gazeti hilo, Elvan Stambuli alisisitiza wito kwa wasomaji  wa magazeti ya Global Publishers ya Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani, na Championi kuendelea kulinunua Uwazi kwa bei ya Sh. 500 kwani thamani ya kilichomo ndani yake ni zaidi ya bei hiyo.

(PICHA/HABARI:  MAYASA MARIWATA/GPL)

Leave a Comment