Watu wanne wamefariki dunia na wengine 49 wamejeruhiwa baada ya treni kuacha njia na kugonga mnara karinu na eneo la O Porrino, Kaskazini Magharibi mwa Hispania.
Takribani abiria 60 walikuwa ni raia wa Ureno na inasemekana miongoni mwa watu waliofariki dunia ni pamoja na dereva wa gari moshi hilo.
Behewa moja limeharibika kabisa huku mwngine mawili yakiwa yamebondeka vibaya.
Vikosi vya uokoaji viliwahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuwaokoa baadhi ya abiria na watumishi wa treni hiyo waliokuwemo ndani wakati likipata ajali karibu na mpaka wa Ureno.
Mnamo Julai 31 mwaka 2013, ajali kama hiyo ilitokea baada ya treni kuanguka karibu na Mji wa Santiago de Compostela, na kuuwa watu 79 huku wengine 170 wakijeruhiwa