×

Swaga za wasanii hawa ni mulemule

prezzo11Na Boniphace Ngumije, Ijumaa:

MITAANI huwa ni jambo la kufurahisha kuona mshikaji au sistaduu f’lani anafanana na staa f’lani au swaga zake zinaendana na staa huyo.

Watu huwa wanajivunia kiasi kwamba wengine hujibatiza au kubatizwa majina ya mastaa hao.

Hata hivyo, mbali na watu wa kawaida hata kwa mastaa nao huwa wana mastaa wao wanaotokea kufanana nao, kugandamizia swaga zao na kupenda kuonekana kama mastaa hao.

Wafuatao ni baadhi ya mastaa ambao wametokea kufanana na wengine na kujikuta swaga zao zikiangukia mulemule.

CMB PREZZO VS BIRDMAN

Cash Money Brother’s President, CMB Prezzo ni rapa asiyekaukiwa na vituko mwenye jina kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki akitokea nchini Kenya.

Mbali na vituko vinavyomfanya asikauke kwenye media, mshikaji huyu ni smati sana na anapenda kuishi maisha ya kinyamwezi huku akiwa amejichora tatuu kibao sehemu kubwa ya mikono yake na shingoni.

Rapa huyu amewahi kukiri kumkubali sana na kuiga ‘life style’ ya rapa ambaye pia ni mfanyabiashara anayemiliki Lebo ya Cash Money Records pamoja na kampuni ya kuuza gesi iitwayo Bronald Oil and GAS, LLC, Birdman.

Kutokana na kumuiga Birdman, Prezzo amefanikiwa! Ukimcheki swaga zake na Birdman utaona wanakwenda sawa.

salama4SALAMA JABIR VS AZMARIE

Salama ni mtangazaji na mdau wa muziki maarufu Bongo. Kwa muonekano wa nje mwanadada huyu ana swaga za kiume mwanzo mwisho. Ni nadra sana kumkuta katupia mavazi ya kike.

Kwa Salama inawezekana kabisa akawa hamzimii mwanadada ambaye ni mwanamitindo na muigizaji maarufu Marekani, AzMarie Livingston aliyetisha kwenye Tamthilia ya Empire. Lakini wawili hawa wanaendana sana kwa swaga.

CASSPER NYOVEST VS SCHOOLBOY Q

Cassper Nyovest ni miongoni mwa Wanamuziki wa Hip Hop wanaopendwa mno Afrika kwa sasa. Nyimbo zake za Shebeleza na Mama I Made It zimempatia mafanikio makubwa ya kimuziki na kufanya ajulikane kila kona duniani.

Staa huyu anaingia kwenye list hii kwa kufanana kiswaga na rapa mwenye asili ya Ujerumani na Marekani, Schoolboy Q aliyetamba na ngoma iitwayo Collard Greens. Ukiwaona washikaji hawa inaweza kukuwia vigumu kuwatofautisha.

young-dee1YOUNG D VS PATORANKING

Wakikutana pamoja utasema ni watoto waliozaliwa na baba mmoja. Washikaji hawa wanafanana sana jambo ambalo hata Young D huwa anajivunia.

Wakati fulani akifanya mahojiano na moja ya magazeti ya Global Publishers ‘kichaa’ huyo wa kurap alisema kuwa yupo kwenye harakati za kumshirikisha Patoranking kwenye ngoma yake moja katika siku za hivi karibuni, pia anamkubali kwa sababu wanafanana na kuendana ‘kiswaga’.

jux-3JUX VS TREY SONGS

Mikato ya staa wa Bongo Fleva ambaye wimbo wake uitwao Wivu ni gumzo kila kona kwa sasa Bongo, Jux ni mulemule na swaga za mkali wa RnB wa Marekani, Trey Songs.

Kwa Jux, Trey ndiye ‘role model’ wake. Amewahi kukiri kwenye ‘interview’ kuwa anamkubali kinoma mshikaji huyo ndiyo maana haoni hata shida kukopi anachofanya kuanzia kujichora tatuu hata mapozi ya picha!

Leave a Comment