×

Video: LSF Yaadhimisha Miaka 5 Ya Mafanikio Yake

halaliiii1

Mkurugenzi wa LSF, Scolastika Juno, (wa pili kulia kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa taasisi zinazotoa msaada wa haki za kisheria na tuzo walizozipata katika hafla hiyo.

halaliiii2

…Mkurugenzi huyo akikata keki kuashiria kutimiza miaka mitano.

halaliiii3

Mkurugenzi Scolastika akiwalisha keki baadhi ya wageni waalikwa.

halaliiii4

Wageni waalikwa wakiendelea kupata keki.

halaliiii5

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo.

Na Hilaly Daud/Gpl

MFUKO ujulikanayo kama Legal Services Facility (LSF)  chini ya Mkurugenzi wake, Scolastika Juno, jana umeadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake na kueleza mafanio yake.

Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya New Afrika  Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wageni wengine waalikwa.

Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Scolastika alisema kuwa lengo la mfuko huo ni kutoa misaada wa kisheria katika mashirikia binafsi  na taasisi nyingine na akaongeza kuwa mfuko huo ulitokana na makubaliano ya Serikali ya Tanzania na watu wa Denmrk baada ya kuanzishwa Desemba 20, 2011.

Alisema, tangu mfuko huo umeanzishwa umeweza kutoa ruzuku ya shilingi milioni 20 kwa mashirikia 43 yanayotoa msaada wa kisheria kwa wananchi.

Aidha, sherehe hizo ziliambatana na utoaji wa zawadi kwa taasisi zilizopo mikoani zenye lengo la kusaidia wananchi upatikanaji wa haki za kisheria.

Kwa habari kamili tembelea Global TV Online.