MWANA – BONGO FLEVA, mkali wa sauti na mashairi, Ali Saleh Kiba ‘king Kiba’ ashinda tuzo mbili za The Nollywood & African Film Critics (NAFCA).
Kiba ameshinda vipengele viwili kwenye tuzo za heshima kubwa za The Nollywood & African Film Critics (NAFCA) ambazo hutolewa nchini Marekani.
Tuzo za mwaka huu zilitolewa wikiendi hii kwenye ukumbi wa Alex Theatre of Glendale, huko California. Zilikuwa ni tuzo za 6 na zilionekana katika nchi mbalimbali duniani.
Alikiba ameshinda kipengele cha Favorite Artist of The Year na Favorite Song of The Year.