KENYA: Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege Kenyan Airways la nchini Kenya, Mbuvi Ngunze amejiuzulu baada ya kufanya kazi na shirika hilo kwa muda wa miaka mitano kufuatia mashinikizo ya muda mrefu kutoka kwa wafanyakazi wa shirika hilo wakimlaumu kwa utendaji wake mbovu.
Uamuzi huu umekuja ikiwa ni mwezi mmoja tangu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Bwana Dennis Awori ajiuzulu.
Wafanyakazi hao walikuwa pia wakiulalamikia uongozi kwa kusababisha baadhi abiria kuchelewesha safari zao.
Shirika hilo lilitangaza jana kuwa, bwana Ngunze ataachia rasmi madaraka yake mwanzoni mwa mwaka kesho ambapo kwa sasa atabaki kuusaidia uongozi wa mpito uliopo.
Source: Standard
