×

Mwanakijiji azua hofu kujenga ghorofa la miti

photo72Na Gregory Nyankaira, Amani

MARA: Juma Wazere, mkazi wa Kijiji cha Singu mwenye umri wa miaka 54, amewapa hofu wenzake baada ya kukamilisha ujenzi wa ghorofa la miti la kuishi yeye na familia yake ya mke na watoto sita, wakidai kutokana na kutokuwa imara, linaweza kuanguka na kuleta madhara.

ghorofaMwanakijiji huyo amejenga nyumba hiyo kwa kutumia miti, kamba za katani, udongo ambao umetumika kukandika pamoja na kuezeka kwa nyasi.

Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, wananchi hao alisema nyumba ni ya kwanza ya aina yake kujengwa katika kijiji hicho na labda  koa mzima wa Mara wanaamini kwa kujengwa kwake kienyeji bila ya kushirikisha wataalamu, haina ubora wa kuhimili uzito wa ghorofa na kuwa huenda ikaanguka baadaye na kuleta maafa katika familia hiyo iwapo serikali haitachukua hatua za haraka kuizuia familia hiyo kuishi humo.

nyumba-juu-ya-mtiNyumba ya kisasa iliyojengwa juu ya mti

“Haya ni maajabu kweli, iweje mtu mzima na akili zake timamu ajenge nyumba ya ghorofa ya miti iliyofungwa kwa kamba za katani, kukandikwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi ili aishi na familia yake, kweli watu wengine hujitakia maafa kwa makusudi na kuilaumu bure serikali na kusababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia kama huyu anavyotaka kufanya sasa,” alisema mkazi mmoja wa kijiji hicho, Makona George.

Lakini Wazere mwenyewe alipuuza madai hayo ya wanakijiji wenzake na kudai amejenga nyumba hiyo kwa ajili ya kudumisha utamaduni wa kiafrika na kwamba tangu mwanzo wazee waliishi na kujenga nyumba za miti zilizokandikwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi japo nyumba hizo hazikuwa na ubora.

“Wazee wetu walijenga nyumba za miti lakini hazikuwa na ubora, hivyo mimi nimeamua kudumisha utamaduni huo kwa kujenga nyumba ya vifaa vya asili na nimeboresha zaidi utaalamu kwa kujenga ghorofa bila kutumia vyuma wala tofali,” alisema Wazere.

Lady Jaydee Amtambulisha Mpenzi Wake Mpya , Agoma Kumsaidia Ray C