×

Mfaransa wa Yanga Afanya Vikao Vitatu Tofauti

umuyobozi-wa-marketing-muri-ferwafa-yasezerewe-_55d1b8835564a-gifAmbaye anatajwa siku za usoni kuja kuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, Jerome Dufourg.

Waandishi Wetu, Dar es Salaam Championi Ijumaa 23.12. 2016

MFARANSA Jerome Dufourg ambaye anatajwa siku za usoni kuja kuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, juzi Jumatano alifika kwenye mazoezi ya kikosi cha timu hiyo na kufanya vikao vitatu tofauti.

Yanga ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru, Mfaransa huyo alikuwa nje ya uwanja akifuatilia hatua kwa hatua jinsi kocha mkuu, George Lwandamina na wasaidizi wake, Juma Mwambusi na Noel Mwandila walivyokuwa wakifanya kazi yao.
Baada ya mazoezi hayo saa 11:30 jioni, Mfaransa huyo alimfuata Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh na kuzungumza naye kwa takriban dakika tano.
Baada ya hapo alimfuata Lwandamina na akazungumza naye kwa dakika moja kisha akamfuata Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la Yanga, Hans van Der Pluijm na kuzungumza naye kwa dakika tano.
Alipomaliza hapo alianza kuwa bize na simu kwa zaidi ya nusu saa kisha mida ya saa 12:20 akaondoka na alipofuatwa na gazeti hili, alisema:
“Nimekuja tu kuangalia mazoezi, lakini bado sijaanza kazi. Siku nikianza kazi nitawaambia na lazima mjue kwani kutakuwepo na mkutano na waandishi wa habari, inaweza kuwa wiki ijayo, wiki mbili zijazo au hata mwakani, usishtuke kusikia mwakani, kumbuka tumebakiza kama wiki moja hivi kuumaliza mwaka huu, hivyo siku si nyingi nitaanza kazi.”
Ikumbukwe kuwa, Mfaransa huyo ambaye aliwahi kufanya kazi katika Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), alitua nchini Novemba 5, mwaka huu kwa ajili ya kufanya kazi na Yanga.

Duh! Hii Kali, Sangoma Anaswa Akimroga Darassa!