
Mashabiki wakiburudika katika ukumbi wa maraha wa Dar Live.
Mwanamuziki wa Jahazi Modern, Prince Amigo, akitoa burudani ya kufa mtu kwa mashabiki.

Baadhi ya waimbaji wakitoa burudani.

Abby Skillz (kulia) akiwa na Amigo, wakitoa burudani.

Baadhi ya wapiga vyombo wakifanya mambo yao.

Mashabiki wakiendelea kuburudika.

Abby Skillz akitoa burudani.
Na Waandishi Wetu/GPL
KUNDI la muziki wa taarab, Jahazi Modern, usiku wa kuamkia leo lilifunika ipasavyo katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar baada ya kudondosha bonge la burudani katika mkesha wa Krismasi.
Kundi hilo lilitoa burudani iliyokonga nyoyo za mshabiki wake, huku nyimbo za Tiba ya Mapenzi, Nina Moyo Sina Jiwe, Nilijua Mpenzi Chocolate na nyingine kibao ziliwafanya wapenzi wa muziki huo wanyanyue vidole juu kwa kila wimbo uliopigwa.
Kiongozi wa kundi hilo, Prince Amigo, alimtambulisha mwimbaji mpya wa kundi hilo, Mariamu, wa BSS ambaye atakuwa kwenye safu ya uimbaji. Aidha msanii wa kizazi kipya, Abby Skillz, naye aliibua shangwe baada ya kulivamia jukwaa na kudondosha ‘mipini’ iliyofanya vizuri.
Wanamuziki wengine waliotumbuiza ni Mosi Suleiman, Amigo, Leila Rashid na wapiga vyombo wakiongozwa na mpiga kinanda maarufu, Ally Jay.