DAR ES SALAAM: Upelelezi wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lisu pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio na mchapishaji wake, umekamilika na sasa shauri hilo litaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 15 mwaka huu.
Kutoka kushoto ni Mmiliki wa Mitambo ya Kuchapisha Magazeti Ismail Mahboob, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, na wahariri wa Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, Lissu alipandishwa pamoja na washtakiwa wenzake, Simon Mkina na Jabir Idrisa ambao ni wahariri wa gazeti la Mawio na mchapishaji Ismail Mahboob ambao kwa pamoja wanatetewa na wakili Peter Kibatala huku Mwendesha Mashtaka wa Serikali akiwa ni Patrick Mwita.
Kutoka kushoto ni Mkina, Tundu Lissu na wakili wao Peter Kibatala wakiondoka mahakamani hapo.
Baada ya kusomewa shtaka lao, wote walikana na hivyo hakimu kuahirisha shauri hilo hadi siku hiyo na kuitaka Jamhuri kupeleka mashahidi wake.
Kutoka kulia ni Mwandishi Mkongwe, Mzee Timoth, Mkina, Idrisa na wakili wao.
Na Denis Mtima/GPL