×

Haya Ndiyo Anayoyafanya Mbunge Ridhiwani Kikwete Akiwa Nyumbani

ridhiwani

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametupia picha mtandaoni ikimuonesha akiwa nyumbani kwake huku akitimiza majukumu yake ya malezi na upendo kwa mwanaye.

Katika picha, Ridhiwani ameonekana akimfumua nywele binti yake, Aziza Tamika Kikwete nyumbani kwake Chalinze mkoani Pwani na kutupia picha hiyo akisindikiza na maneno haya Instagram:

“@home attending Fatherhood duty while watching H.E Donald Trump taking Oath of the Office.” Akiwa na maana kwamba anatimiza majukumu kama baba huku akimuangalia Donald Trump akila kiapo cha kuingia ofisini (ikulu).

ridhiwani

Kwa namna moja ama nyingine jambo hilo ni la kuigwa kwani Ridhiwani kupitia picha na maneno aliyoandika amewahimiza akina baba wengine kuwa karibu na watoto wao na kuwasaidia kwa kila jambo wanalohitaji kutoka kwa wazazi wao hasa wa kiume ili kuhakikisha wanakuwa katika malezi yaliyo bora na wafikie malengo yao.