MSIMU wa pili wa bahati nasibu ya Shinda Nyumba iliyozinduliwa hivi karibuni na Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Risasi, Amani, Championi, Ijumaa Wikienda na Ijumaa unazidi kushika kasi huku wasomaji mbalimbali kutoka kila kona ya nchi wakijipatia magazeti ya Global na kukata kuponi.

Afisa Usambazaji wa Global Publishers, Kefa Masaga (aliyekaa), akimsaidia Aisha Issa, mkazi wa Magomeni Mikumi kujaza kuponi ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Afisa Usambazaji wa Global Publishers, Jimmy Haroub (mwenye kofia nyekundu) akimpa maelekezo Ivan Moses, mkazi wa Kivule jinsi ya kujaza kuponi baada ya kununua Gazeti la Amani linalotoka kila Alhamisi.
Jimmy Haroub akizungumza jambo na mteja wa magazeti ya Global Publishers, Isaya Stephano Emmanuel, mkazi wa Kitunda baada ya kukata kuponi.

Jimmy Haroub (mwenye kofia nyekundu), akimjazia kuponi Aziza Juma, mkazi wa Kivule baada ya kukata kuponi.

Jimmy Haroub (kulia) akizungumza na Paul Mray, mkazi wa Kivule baada ya kukata kuponi ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

Kefa Masaga (aliyesimama), akimsaidia kujaza kuponi Pandu H. Pandu, mkazi wa Kivule baada ya kukata kuponi kwenye Gazeti la Amani. 
Wasomaji wa magazeti ya Global Publishers, ambao ni wakazi wa maeneo yanayolizunguka eneo la Airport wakiwa kwenye picha na Afisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroob baada ya kukata kuponi. 
Jimmy Haroob (kushoto), akimpa maelekezo Peter V. Mbise, mkazi wa Kivule namna ya kujaza kuponi
Leo, bahati nasibu hiyo imetinga mitaa ya Kivule jijini Dar es Salaam ambako wasomaji mbalimbali walijitokeza na kuchangamkia fursa kwa kununua magazeti na kukata kuponi ili kujishindia nyumba na zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki na vyombo vya maakuli (dinner set) katika droo mbalimbali zitakazokuwa zinachezeshwa kila mwezi.
NA BONIPHACE NGUMIJE/GPL