


Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni saba laki tano na elfu tisini na mbili (7,592,000/= ) za afya halmashauri ya siha, walinzi wa shamba la miti West Kilimanjaro na shule ya sekondari Magnifikacant na za mama lishe Bi Fatuma zilizokuwa zimedhulumiwa na kufanyiwa ubadhirifu na watuhumiwa ambao ni aliyekuwa mhasibu wa halmashauri na mlinzi mkuu wa shamba.
Zoezi la kukabidhi fedha hizo limefanyika mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Onesmo Buswelo, ambapo kabla ya kupata taarifa za ubadhirifu huo taasisi hiyo ilianza uchunguzi ambapo baada ya kuwahoji watuhumiwa wote walikiri kufanya makosa hayo hivyo kuamuriwa kurudisha fedha hizo.
Mkuu wa wilaya ya Siha, Onesmo Buswelo licha ya kuipongeza TAKUKURU kwa kazi hiyo ameonekana kukerwa na kitendo hicho na kuamuru mtuhumiwa Christopha Ngonyani na Namson Fisso licha ya kurudisha fedha hizo kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo.
Baadhi ya wananchi na watumishi ambao walidhulumiwa fedha zao kwa hila na udangayifu wameishuruku Taaisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kufanikisha zoezi hilo huku wakiwashauri wananchi wengine kutoogopa kuitumia taasisi hiyo kuibua watu wengine wenye vitendo viovu kama hivyo.
Watu waliodhulumiwa fedha zao ni watumishi 126 wa idara ya afya, walinzi 8 wa shamba la miti West Kilimanjaro, shule ya sekondari Magnificant, mama lishe, Embassy Tea room zote za wilayani Siha zilizokuwa zimefanyiwa ubadhirifu na watuhumiwa Namson na Ngonyani aliyekuwa mhasibu halmashauri ya siha na mlinzi mkuu wa shamba la misitu la West Kilimanjaro.