×

Simba: Tutawapiga Azam kipigo mujarabu

azam-na-simba-3

Na Mwandishi Wetu | CHAMPIONI

WAKATI presha ya mchezo kati ya Simba na Azam ikiwa kubwa, Kocha wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, ameweka bayana kwamba hana hofu kwa kuwa anaamini kikosi chake kitaibuka na ushindi mujarabu bila kuwa na ugumu wowote.

Simba wenye pointi 45 wakiwa kileleni watakuwa na kibarua cha kupambana na Azam wenye pointi 31, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, kesho Jumamosi katika Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe mchezo uliopita katika ligi hiyo, Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Shiza Kichuya.

“Hatuna hofu hata kidogo licha ya kwamba watu wanaliona pambano hilo ni kubwa, ila sisi tunauchukulia kama mchezo wa kawaida sawa na ile ya siku zote tunapocheza na timu nyingine za ligi,” alijinadi Omog na kuongeza:

“Mara ya mwisho walitufunga (katika Mapinduzi Cup) lakini safari hii hatutaki kuona jambo hilo linajitokeza tena na isitoshe kipindi hiki tunazihitaji pointi zao ili tubaki kileleni na kuwakimbia wapinzani Yanga wanaotufuatia.”

Aidha, upande wa Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche, alikuwepo uwanjani Jumapili iliyopita kuishuhudia Simba ikicheza na Polisi Dar katika FA Cup ambapo alionekana kuwa makini mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam