×

(+Audio): Mtangazaji wa Runinga Anusurika Kuporwa Gari, Atoa Somo!

mtangazaji-3STORI: IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Style and Profile kinachorushwa kupitia Televisheni ya Channel 10, Zeiny Aklan (pichani) amekumbwa na kizaazaa cha aina yake baada ya hivi karibuni kunusurika kuporwa gari yake aina ya Toyota Noah alipokuwa akitoka Hospitali ya Mikumi-Magomeni jijini Dar, kuchoma sindano.

Zeiny ameliambia Gazeti la Risasi Jumamosi kuwa, anamshukuru Mungu kwanza kwa kuwa yupo salama lakini siku hiyo ilikuwa mbaya na kama asingekuwa makini, huenda hadi sasa asingekuwa na gari hilo.

Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, Zeiny alisema siku ya tukio, majira ya saa nane mchana, alienda hospitali ambapo alipofika, alipaki gari lake nje ya hospitali hiyo na kuingia ndani kutibiwa.

“Baada ya kuhudumiwa, nilipotoka, nikaelekea kwenye gari langu, nilipofika nilimkuta kijana mmoja amekaa nyuma ya gari langu,” alisema Zeiny na kuendelea kueleza kwamba baada ya kufungua mlango na kuwasha gari lake, yule kijana alimfuata na kumwambia kwamba ana shida hivyo anaomba amsikilize.

mtangazaji-1

Zeiny anaeleza kuwa kijana huyo alizidi kumsogelea mpaka akamkaribia kabisa lakini ghafla wakatokea vijana wengine kati ya wanne au sita, wakawa wanamzonga ambapo mmoja aliongea kwa sauti kwamba ampokonye ufunguo wa gari.

“Niliposikia hivyo sikupaniki, nikajifanya kama nimesahau simu ndani ya hospitali kwa hiyo nilifunga mlango wa gari kwa nguvu na kukimbilia hospitalini, kwa bahati nzuri funguo yangu huwa ina remote kwa hiyo nikafunga gari kwa mbali na kukimbilia mpaka ndani ya hospitali bila yule kijana kuelewa kwamba nimemshtukia,” alisema Zeiny na kuendelea kueleza jinsi mkasa huo ulivyoendelea na jinsi alivyosaidiwa na wasamaria wema na kunusurika kuporwa gari lake au kufanyiwa uovu mwingine.

Msikilize Zeiny akisimulia mkasa mzima kwa kubofya hapo chini:

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam