×

Bill Nass Ajitabiria Makubwa

       

Bill Nas

RAPA anayekimbiza Bongo, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake kipya kiitwacho Mazoea, Bill Nass amejitabiria makubwa katika kazi zake kwani hivi sasa yupo bize kuboresha anachokifanya na miaka miwili ijayo, atakuwa wa kuogopwa Bongo.

Akichonga na Risasi Vibes, Bill Nass alisema kuwa ni kweli kwa sasa anafanya vizuri na pia ni miongoni mwa marapa wakali, lakini bado hajafikia ndoto zake za kuwa mkali kuliko wote.
“Ukiangalia kazi zangu ninazofanya, ni za viwango vya juu, nipo kwenye ushindani mkali na marapa wanaofanya vizuri pia, lakini ndani ya miaka miwili mbele nataka niwe rapa ambaye sina mshindani, niwe juu yao wote hapa Bongo,” alisema Bill Nass

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save