Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala, ametoa maagizo mazito kwa Vyombo vya Usalama nchini kuhakikisha vinamkamata mtu anayejulikana kwenye mitandao ya kijamii kama James Delicious kufuatia kujitangaza kwake kama shoga kinyume cha sheria ya Tanzania.
Dk. Kigwangalla ametoa kauli hiyo jana jioni mjini Dodoma Bungeni wakati akijibu hoja za wabunge juu ya hatua kwa mtu anayefanya vitendo hivyo ambapo ameviagiza vyombo vya usalama kumtafuta mtu huyo na iwe fundisho kwani ni kinyume na sheria za nchi kwa kuendesha biashara ya kuuza ngono ya kinyume cha maumbile.
Mbali na James Delicious, wengine ambao ameagiza wajisalimishe wenyewe kituo cha Polisi Central Dar es Salaam ni pamoja na Kaoge Mvuto na Dani Mtoto wa Mama ambao wamekuwa wakijinadai kufanya vitendo hivyo hapa nchini ambavyo ni kinyume na sheria.