
BAADA ya jana jina lake kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kutakiwa kufika kesho katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Central’, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima, Daktari Josephat Gwajima amejibu wito huo kuwa Makonda alipaswa kumtumia samasi.

Akizungumza na waandishi wa habari kanisani kwake mchana huu, Gwajima alisema wakati taarifa hizo zinatoka hakuwa karibu na vyombo vya habari na kwamba alikuwa njiani na Helkopta akielekea Mpwapwa katika moja ya makanisa yake.

Askofu wa Kamati ya Maadili Tanzania, Wilkliam Mwamalanga aklizungumza jambo.
“Nilipokuwa njiani nikapigiwa simu na kuambiwa kuwa ninametajwa na Makonda katika watu wanaotuhumiwa kutumia madawa. “Kwanza ningependa nimwambie tu Makonda, alipaswa kuniletea samasi au kunipigia simu.

Waumini wakimsikiliza Gwajima.
Si mara moja tunawasiliana naye na hata mara ya mwisho alikuja katika kanisa langu hapa akiwa na Mwakyembe na Samuel Sitta kuombewa DVD zake ninazo, mbona hakuniambia kuwa nahusika na madawa ya kulevya?
Askofu Deo Lilanga akizungumza.Gwajima aliyekuwa ameambatana na baadhi ya maaskofu aliendelea kusema kuwa, anamsifu sana Makonda kwani ni mtu jasiri na mwenye uthubutu na anaweza kuwa mtu mkubwa hapo baadaye.
Gwajima akionesha picha aliyopiga na Makonda.“Nimekuwa mchungaji kwa zaidi ya miaka 20, napambana kila siku nifanikiwe na mali nilizonazo ni kutokana na jasho langu. Mimi ni daktari wa Filosofi na ni kati ya madaktari wachache sana nchini. Naitwa kila mara nje ya nchi kwenda kufundisha. Kufundisha huko lisaa moja tu kwa mwanafunzi nachukua dola 1,000 (zaidi ya milioni 3) sasa piga hesabu nafundisha wanafunzi wangapi na mara ya mwisho nilikuwa Japani miezi mitatu nikifundisha,” alisema Gwajima.

Gwajima akipanda gari na kuondoka kuelekea Sentro.
Naye Askofu Mkuu wa Kamati ya Nidhamu, William Mwamalanga alisema waliwahi kupokea malalamiko kwa mtu kuwa Gwajima anajihusisha na madawa lakini walipomchunguza walibaini ni uongo.
“Tuliwahi kumchunguza Gwajima kwa miezi mitatu lakini mwisho wa siku tukajua kuwa ni uongo na yule aliyetuambia kwa aibu akamfuata Gwajima na kuomba aombewe,” alisema Askofu Mwamalanga. Hata hivyo baada ya Gwajima kuzungumza na waandishi, alielekea moja kwa moja Central kuitikio wito huo.
STORI: NA ANDREW CARLOS | Dennis Mtima | Kelvin Shayo | GLOBAL PUBLISHERS