×

Maadhimisho ya Utamaduni wa Washirazi na Watanzania Yafanyika

Baadhi ya raia wa Iran waishio hapa nchini wakiimba nyimbo za kwao.

Raia wa Iran wakijadiliana jambo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ambapo ndipo yanapofanyika maadhimisho hayo.

Baadhi ya wananchi waliofika katika ukumbi huo wakiangalia baadhi ya bidhaa zilizokuwemo

 

Mfanyabiashara wa vitabu, akisubiri wateja.

Sehemu ya vinyago vya asili vilipokuwa.

WANANCHI mbalimbali wa Tanzania leo wamejumuika na wenzao wa Iran (Washirazi) kwenye Makumbusho ya Taifa, Posta jijini hapa kunakofanyika maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi wa Iran na Watanzania.

Maadhimisho hayo yaliyoanza Februari 10, 2017 na kutarajiwa kufika kilele chake kesho Februari 12, 2017 yakijumuisha maonesho ya bidhaa na shughuli mbalimbali za kiutamaduni, mwaka huu yanaenda kwa kauli mbiu ya Ushirikiano wa Kiutamaduni ni Nguzo Muhimu ya Kukuza na Kuendeleza Lugha, Mila na Desturi Zetu.

NA DENIS MTIMA/GPL