
HAMISA Mobeto; ni mwanamitindo wa kimataifa, msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali ambaye moja ya mambo anayoyapenda ni pamoja na kuonekana mrembo hasa kwenye mitandao ya kijamii ambako huko ndiko hujipatia madili kibao ya ubalozi.
Kwa muda mrefu, wafuasi wa Hamisa wameamini kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na rapa wa Marekani, Rick Ross, lakini hapo katikati ni kama mawasiliano yalikatika baada ya kukutana na kuachana kule Dubai mwishoni mwa mwaka jana.

Hata hivyo, mawasiliano yamerejea na wanaendelea pale walipoishia baada ya kuanza kusifiana kwenye kurasa zao za Instagram.
Hii ni baada ya juzi Hamisa kuposti picha yake matata ambapo Rick Ross alikuwa wa kwanza kuweka maoni akimuita Hamisa; ‘my baby’ huku Hamisa akijibu mapigo; ‘I miss you’.
STORI: SIFAEL PAUL