
Shentee Muroz
MUBASHARA! Lile shindano linalendeshwa na Gazeti la Ijumaa Wikienda la unataka kuwa msanii mkubwa wa muziki kupitia Wikienda Music Search (WMS), linatarajia kuanza rasmi Jumatatu ijayo.
WMS ambayo inadhaminiwa na Mtayarishaji wa Muziki wa Bongo Fleva, Shentee Murozy itaanza Jumatatu ijayo ambapo kila mshiriki aliyejana kuponi na kufikisha ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga Mwenge, jijini Dar basi atatumia SMS ya muda na mahali pa kufanyia usaili.

“Jumatatu ijayo ndiyo tunaanza mashindano rasmi, kwa wale walionunua Gazeti la Ijumaa Wikienda na kujaza kuponi ya WMS na kuifikisha ofisi za Global. Pia wasomaji wanaweza kudownload wimbo wangu mpya wa Feeling kupitia You Tube ili kuona ubora wa kazi tuzifanyazo kupitia studio yetu ya Black Iliyopo Mgaomeni Kagera, jijini Dar,”alisema Shentee Murozy