×

Mpelelezi Makao Makuu Atoa Ushahidi Kesi ya Malkia Meno ya Tembo

DAR ES SALAAM: KESI inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan (66) almaarufu Malkia wa Meno ya Tembo leo imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu ambapo ushahidi umeendelea kutolewa na upande wa jamhuri.

Malkia  wa Meno ya Tembo alipofikishwa mahakamani Kisutu, leo.

Aliyetoa ushahidi leo alikuwa ni Koplo Emmanuel wa Idara ya Upelelezi Makosa ya Jinai Makao Makuu ya Polisi (Sentro) ambapo aliieleza mahakama juu ya kile anachofahamu juu ya kesi hiyo.

Shahidi huyo ametoa maelezo yake mbele ya Hakimu Mkuu,Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ambapo alieleza mambo mbalimbali yanayohusu kesi ya mtuhumiwa huyo.Kesi hiyo itaendelea kesho tena kusikiliza upande wa mashahidi.

Glan anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara Salvius Matembo (39) na Manase Philemon (39) ambapo inadaiwa kwamba kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali bila kibali.

Katika kipindi hicho wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 vyenye thamani ya shilingi 5.4 bilioni bila leseni iliyotolewa na mkurugenzi wa wanyamapori.

STORI NA DENIS MTIMA|PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Save

Save