Miaka 10 ya Jahazi... Amigo Kuimba Nyimbo 3 za Mzee Yusuf Dar Live - Global Publishers
Imewekwa na on February 17th, 2017 , 05:49:13pm

Miaka 10 ya Jahazi… Amigo Kuimba Nyimbo 3 za Mzee Yusuf Dar Live

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuelekea kutimiza miaka 10 tangu Kundi la Muziki wa Taarab nchini, Jahazi Modern lianzishwe, mkali wa Wimbo wa Tiba ya Mapenzi, Prince Amigo amefunguka kuwa, siku hiyo (Februari 25) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, ataimba nyimbo tatu zilizowahi kuimbwa na muasisi wa kundi hilo, Mzee Yusuf.

Akizungumza na Burudani Jumamosi jana katika mahojiano na Global TV Online, Amigo ambaye ndiye kiongozi wa kundi hilo tangu Mzee Yusuf aliache na kuingia kwenye dini alisema, nyimbo hizo atakazoimba ni Tupendane, Anajua Kupenda pamoja na Kaning’ang’ania.

“Tangu Mzee Yusuf aliache kundi hili hatujawahi kutetereka na niwaambie tu mashabiki wote wa burudani waje kwa wingi kwani mbali na kupiga nyimbo hizo, pia tutakuwa na wanamuziki wote waliowahi kupitia Jahazi tangu limeanzishwa,” alisema Amigo.

Nyimbo nyingine zitakazotingisha usiku huo ni pamoja na Tiba ya Mapenzi, Nina Moyo Sio Jiwe, Mpenzi Chocolate, Kwa Hilo Hamjanikomoa na nyingine kibao kwa kiingilio cha shilingi 8,000 tu.

 

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma