Global Updates: Hatimaye Alikibwa Akibidhiwa Tuzo Yake Ya MTV EMA
Imewekwa na on February 17th, 2017 , 03:28:15pm

Global Updates: Hatimaye Alikiba Akabidhiwa Tuzo Yake Ya MTV EMA: Best African Act 2016

Kwa wale mashabiki wa King Kiba Alikba, good news ikufikie kuwa hatimaye Alikiba amekabidhiwa ile tuzo yake ya MTV EMA: Best African Act ambayo ilitolewa kimakosa kwa Wizkid, msanii wa muziki kutoka Nigeria.

Alikiba ambaye bado anatamba na wimbo wake wa ‘Aje’ amekabidhiwa tuzo hiyo nchini Afrika Kusini alikoenda kwaajili ya ziara yake ya huko. Kupitia page yake ya Instagram @officialalikiba, staa huyo wa Bongo Fleva ameandika ujumbe mfupi wa shukrani kwa management yake. Ujumbe huo umesema:

“I would like to thank God for the continuous blessings, my family, my management and the fans. I love you all endlessly !!#MTVEMABestAfricanAct #KingKiba,”

Baada ya taarifa rasmi ya MTV EMA, kuhusu ushindi halali wa tuzo hiyo kwa Alikib, Alikiba alipost ujumbe mwengine unaosema:

Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania 🇹🇿 pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana #bloodfanswaalikiba #Kajiandae #KingKiba

Aliongeza,

“Ningependa pia kuchukua nafasi hii kushukuru vyombo vya habari vyote, watangazaji, waandishi na wadau wote wa sanaa kiujumla kwa kunisapoti katika kazi zangu.

Lastly, nawashukuru wasanii wenzangu wote mlionipa ushirikiano na kuthamini kipaji changu kwa kuniombea kura zilizonipa ushindi. Ushindi wangu ni ushindi wa sanaa yetu sote. Proudly Tanzanian 🇹🇿
MUNGU awabariki sana. #TupoPamoja #Kajiandae #KingKiba

Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania 🇹🇿 pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote – nawapenda sana#bloodfanswaalikiba #Kajiandae#KingKiba”

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma