Yaliyojiri Mahakamani Kisutu Kesi ya Masogange - Global Publishers
Imewekwa na on February 17th, 2017 , 07:42:52pm

Yaliyojiri Mahakamani Kisutu Kesi ya Masogange

Ndugu wa Agness Grald ‘ Masogange’, aitwae Efrans akiwa kwenye viunga vya Mahakama ya Kisutu kumsubilia nduguye ambaye ilikuwa afikishwe mahakamani hapo leo.

Ndugu wakibadilishana mawazo wakati wakisubili kuletwa kwa Masogange.

……Wameschoka sasa wakaamua kulala.

….Wakikata tamaa na kuondoka mahakamani hapo.

…Wakijadiri kabla ya kuingia kwenye gari na kuondoka.

Agness Gerald ‘Masogange’

KIMUHEMUHE kilitanda kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo  Feb 17, 2017, kufuatia ndugu, jamaa na marafiki wa model, Agness Masogange kufurika huku wakitarajia kumuona ndugu yao huyo akifikishwa mahakamani hapo .

Ndugu hao waliwasili Kisutu mapema asubuhi na kuweka kambi mahakami ili kusikiliza kesi ya masogange anayehusishwa na tuhuma za matumizi ya dawa za kuleya.

Licha ya Masogange kutokufikishwa mahakamani hapo kwa kile kinachodaiwa kuwa majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu kipimo endapo mwanadada huyo anatumia madawa ya kulevya, kilikuwa hakijatoka lakini mpaka ilipotimu majira ya saa 9:00 mchana, ndugu hao walikuwa hawajakata tamaa. Baada ya kuona hakuna dalili zozote kwa ndugu yao kuletwa mahakamani hapo huku muda wa mahakama wa saa 9:30 ukiisha, ndipo ndugu hao waliamua kuondoka kwa unyonge eneo la Kisutu.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamnada wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Kamishna Somon Sirro ilieleza kuwa, Masogange na wenzake 17, wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kuhusika na matumizi ya dawa za kulevya, na kwamba jana walipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serkali kwa ajili ya vipimo na endapo ikibainika wanatumia madawa ya kulevya, leo Ijumaa au Jumatatu ijayo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma