×

SADC kuzungumzia Mgogoro wa Kongo na Lesotho, Dar

Mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi wanachama SADC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga akizungumza na wanahabari.

JUMUIYA ya Nchi Za Kusini Mwa Afrika, SADC leo na  kesho kuzungumzia suala la mgogoro uliopo miongoni mwa nchi hizo mbili za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lesotho zinazokumbwa na mgogoro wa kisiasa kama njia ya kuweza kuziwezesha nchi hizo kuondokana na migogoro hiyo.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dk.Stergomen Lawrence akizungumza jambo.

 

Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ukihusisha mawaziri kutoka nchi 15 za jumuiya hiyo.

Akizungumza na wanahabari, mwenyekiti wa jumuiya hiyo hapa nchini, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki, Balozi  Augustine Mahiga alisema kuwa, mbali na kuzungumzia migogoro inayozikumba nchi hizo pia alisema watajadili ajenda iliyoletwa juu ya nchi mbili zilizoomba kujiunga na SADC ambazo ni Comoro na Burundi.

Baadhi ya mawaziri kutoka nchi za jumuiya ya SADC waliohudhuria mkutano huo.

NA DENIS MTIMA/GPL.