×

Msanii Aanika Kichapo cha Msumbiji

Stori: GLADNESS MALLYA | RISASI JUMAMOSI | DAR ES SALAAM

DAR ES SALAAM: Kutokana na sekeseke la Watanzania waishio Msumbiji kurudishwa nchini kutokana na kutokuwa na vibali huku wengine wakidaiwa kufanyiwa vitendo vya kikatili, msanii wa Bongo Muvi, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ameelezea kichapo alichopata nchini humo, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.

Akizungumza na Risasi Jumamosi , Vai wa Ukweli ambaye alidai alikuwa nchini humo kwa ajili ya biashara zake alisema kutokana na vurugu kubwa iliyokuwepo ilibidi akurupuke ghafla na kukimbia kurudi Bongo lakini kabla hajatimiza lengo lake alikutana na kichapo huku akipoteza vitu vyake vya thamani.

Aliendelea kusema kutokana na vurugu hizo huku wanawake wengi wakifanyiwa vitendo vya ukatili alijikuta akiporwa simu yake ya kisasa aina ya I phone six pamoja na fedha zaidi ya shilingi lakini nane.

“Yaani nimekoma na sitarudia tena kwenda Msumbiji maana kichapo cha huko hakisimuliki, kuna fujo hatari na watu wanafanyiwa vitendo vya kikatili yaani nimeponea chupuchupu ninamshukuru Mungu sana kwa kweli kwa kufika salama Bongo.

“Nimeporwa vitu vyangu kwenye fujo hizo ikiwemo simu na fedha, ukweli ile ilikuwa ni kama vita maana tulipewa siku tano za kuondoka ikawa ndiyo kama fujo zimefunguliwa kwani kila mtu alikuwa anafanya harakati zake huku wengine wakikamatwa na kuwekwa mahabusu, nilikurupuka haraka na kupanda ndege kurudi hiyo ikawa ndiyo usalama wangu,” alisema Vai wa Ukweli.