
FBI imemtaja mshambuliaji wa mauaji ya kutisha kuwa ni Shamsud-Din Jabbar mwenye umri wa miaka 42 – mwanajeshi mkongwe na raia wa Marekani kutoka Texas.
FBI ni kifupisho cha Federal Bureau of Investigation yaani Kitengo cha Uchunguzi cha Polisi Marekani.
Shirika la Utangazaji la Uingereza- BBC limetaarifu kuwa Jabbar alikuwa amefanya kazi katika majukumu mbalimbali katika Jeshi la Marekani, ikiwa ni pamoja na katika kitengo cha rasilimali watu na teknolojia ya mawasiliano (IT).
Alipelekwa Afghanistan kuanzia Februari 2009 hadi Januari 2010.
Katika video ya YouTube iliyotumwa mwaka wa 2020, Jabbar alisema kuwa wakati wake jeshini ulimfundisha “maana ya utumishi bora na maana ya kuwa msikivu na kuchukulia kila kitu kwa uzito, ili kuhakikisha kuwa mambo yanafanyika bila kasoro”, CBS inaripoti.
Alisoma katika Chuo Kikuu cha George State kuanzia mwaka 2015 hadi 2017, na kuhitimu shahada katika Mifumo ya Mawasiliano ya Kompyuta.
CBS inaripoti kuwa alioa mara mbili. Ndoa yake ya kwanza iliisha mnamo 2012 na ya pili ilidumu kuanzia mwaka 2017 hadi 2022.
Jabbar alikuwa na rekodi ya uhalifu, inayohusiana na makosa ya barabarani na wizi. Bada ya kutekeleza mauaji hayo, alijiua.
Rais wa Marekani Joe katika hotuba ameliita shambulio hilo kuwa ni “la kuchukiza”.
“Kwa familia zote za wale waliouawa, kwa wale wote waliojeruhiwa, kwa watu wote wa New Orleans ambao wanaomboleza, nataka mjue nina huzuni pamoja nanyi,” asema.
Rais Biden pia alisema wachunguzi wanachunguza iwapo shambulio la New Orleans linahusishwa na mlipuko wa lori uliotokea nje ya Hoteli ya Trump iliyopo Las Vegas saa chache zilizopita.
Stori na Elvan Stambuli | GPL