
Promosheni ya Infinix kali kuliko imezinduliwa ikiwa ni ndani ya mwezi mzima kuanzia tarehe 1 hadi 30 Agosti.

Uzinduzi huo ambao umeambatana na zawadi balimbali zitakazotolewa endapo utanunua simu, pamoja na utengenezaji wa simu hizo endapo zitapata tatizo lolote

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Infinix Meneja wa Promosheni hiyo, Joseph Vigambo amesema kuwa kutakuwa na zawadi mbalimbali zitatolewa endapo mteja atanunua simu za Infinix zikiwemo NOTE 10, HOT 10T, HOT 10i na HOT 10play ambazo moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo.

“Huu ni mwezi wa Infinix ambao zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wateja wetu ambao watanunua simu za Infinix na zawadi hizo zitakuwepo kubwa ambazo ni Tv inch 55, Ps5 na Laptops hizi zitatolewa kwa mshindi wa mwezi mzima na katikati ya wiki kuna droo ndogo ndogo ambazo zawadi zake ni rice cooker, na vitu vingine vingi.

“Pia promosheni hii inalenga kwenye michezo hivyo basi kwa mwezi huu tumechagua mchezo wa danadana ambapo mshindi atapatikana kwa mtu yoyote kuchukua video akiwa anacheza na kisha kututumia kwenye mitandao yetu na kutu‘tag’ tutaona na mshindi atakaye piga danadana nyingi kuliko wengine atajipatia zawadi ya simu ya Infinix, “amesema.
Nae msimamizi wa mkoa wa Carlcare Neema Kennedy amesema kuwa wao wanashughulika na utengenezaji wa simu endapo zitapata tatizo.
” Kutakuwa na ofa ya screen endapo itavunjika ndani ya mwezi huu endapo ukinunua simu kioo kikavunjika utatengenezewa bure, na pia endapo itakiwa na shida yoyote tutakutengezea pale unaponunua simu ukinunua na warrant card ambayo itasaidia kutengeneza simu yako endapo itapata tatizo lolote ndani ya miezi sita”, amesema.
Aisha Karupa ambaye ni Afisa uhusino kutoka Infinix nae amezungumzia promosheni hiyo kwa kusema kuwa Infinix kila mwaka huwa na mwezi wa kuuza na kujuana na wateja wao.
“Mwezi huu ni mwezi wa promosheni hii kali kuliko ambayo itakuwepo mwezi mzima, na kikubwa katika uzinduzi huu ni si kuuza tu bali ni kujuana na wateja wetu na kujua matatizo yao ili tuweze kuyatatua na watuambie wapi tunakosea na wapi tufanye marekebisho.
“Pia kutakuwa na mchezo wa danadana ambapo kwa mwezi huu tutakuwa na balozi wetu, Meena Ally ambaye ndie atakuwa muhamasishaji kwa upande huwo hivyo basi unachotakiwa kufanya ni kupiga danadana na kututumia katika mitandao yetu ya kijamii mshindi atajipatia zawadi kutoka Infinix na zawadi hizi zitakuwepo katika maduka yote ya Infinix Tanzania nzima”, amesema.