×

Makonda: Rais Magufuli Atazindua Ujenzi wa Fly-Over Ubungo, Jumatatu (VIDEO)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefanya mkutano na waandishi wa habari na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambapo amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli, atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu (fly-over) eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam, ambapo ataweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi huo Jumatatu ya Machi 20, 2017.

Fly-over hiyo inatajwa kwamba itapunguza kero ya msongamano wa magari eneo la Ubungo na sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam.

RC Makonda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo.

TAZAMA VIDO MAKONDA AKIZUNGUMZA