×

Kabila la Wala Watu-12

Wanaokula nyama za watu waliona bora miili wale wao kuliko kuoza na kuliwa na funza!

ELVAN STAMBULI NA MTANDAO | UWAZI | SIMULIZI

Naendelea kusimulia simuli­zi ya kweli kuhusu makabila ya Papua New Guinea ya­nayokula nyama za watu; endelea.

MAKABILA ya­nayojulikana kula nyama ya watu ni Wakorowai na Wafore ambao huishi katika milima au miinuko.

Wafore walikuwa hawaju­likani duniani hadi mwaka 1950 baada ya watafiti kuwa­fanyia utafiti huku watafiti hao wakiwa kwenye hatari ya kuuawa na kuliwa miili yao.

Wakati wa utafiti huo, waligundua kuwa watu hao walikuwa wakila wenzao waliokuwa wakifariki, hivyo kujikuta wakikumbwa na maradhi yaliyoitwa ugonjwa wa kifo cha kucheka yaani laughing death.

Ugonjwa huo uliua wa­nawake na watoto wengi kutokana na kula nyama za watu.

Walikuwa wanakula miili ya wenzao waliokufa, badala ya kuwazika, wakawafanya kitoweo kwa madai kwamba walikuwa wakiwaokoa wap­endwa wao hao ili wasiliwe na funza pindi watakapooza.

Nyama ya miili ya watu walikuwa wakiita ‘nyama ya nguruwe mrefu’ yaani Long pig.

Wafore walisema ni bora miili hiyo ikaliwa na wao na ikae kwenye matumbo yao badala kuliwa na funza kwa madai kwamba roho zao zi­tazidi kuishi kwenye matum­bo hasa ya wanawake.

Kwa imani hiyo, wa­nawake walikuwa wakipewa ubongo waupike na kuula kisha nyama kutengenezwa ‘rosti’, hivyo kula na watoto wao.

Hata hivyo, ulaji huo wa miili ya wenzao pamoja na ubongo ulifanya wapate maradhi ambayo waliyaita kwa kabila la kwao kuru na uliua watu wengi wa jamii hiyo. Mtu aliyekuwa akipata ugonjwa huo alikuwa ana­poteza nguvu na kushindwa kutembea kisha mwili ku­konda.

Mtafiti aliyeitwa Dk. Jekly alisema kilichokuwa kiki­sababisha maradhi hayo siyo bakteria au virusi isipokuwa protini iliyokuwa kwenye ubongo wa maiti ambayo ikiliwa ilikuwa inaharibu ubongo kwani ilikuwa ina­sababisha kucheza au kutik­isika na kuharibika, jambo ambalo kitaalamu huitwa brain’s cerebellium.

Ugonjwa huo uliwaan­dama watu hao wala miili ya watu hadi mwaka 2009 am­bapo mtu mmoja aliripotiwa kufariki dunia kwa maradhi hayo.

Lakini tukio baya lilitokea Julai, 2012 ambapo watu 29 wa makabila hayo waliwala watalii kwa kupika miili yao huku wanaume wakitengen­eza supu, sehemu ‘nyeti’ na ubongo.

Kitendo hicho kilisababi­sha serikali kuingilia kati na kwa mujibu wa Gazeti la The Nationa Newspaper la huko, Kamanda wa Polisi Madang, Anthony Wagambie alithibi­tisha hayo.

“Huwa hawafikirii kwamba wanafanya kitu kibaya, wanakiri hayo waliy­oyafanya waziwazi,” alisema kamanda huyo kwa njia ya simu.

Alisema wauaji wa­naamini kuwa wal­iowaua walikuwa wachawi ambao kwa kabila lao huitwa Sangu­ma na kwamba walikuwa wak­iwapa kilevi wenyeji huku wakifanya nao mapenzi wa­navijiji maskini kwa njia ya ki­shirikina.

Kwa kula viungo vya bin­adamu waganga wao walikuwa wana­waambia kuwa wata­pata nguvu ya ajabu na kwamba hata wakipigwa risasi, hazitaingia kwenye miili yao.

Kamanda Wagambie al­isema waligundua kulikuwa na kundi la watu kati ya 700 na 1,000 wa vijijini Kaskazini Mashariki ambao walikuwa wana imani hiyo.

Alisema walikamata watu 28, wake kwa waume na aliwapandisha mahakamani kujibu tuhuma za mauaji ya binadamu wenzao. Wakipa­tikana na kosa watahuku­miwa adhabu ya kifo.

Akasema watuhumiwa wote waliwaweka rumande na kuendelea kuwatafuta wengine waliokula nyama za watu.

Anasema watu hao wali­fanya ukatili mkubwa kwa kuwaua watalii saba na anaamini kwamba walikula miili yao.

Itaendelea wiki ijayo, usikose mwendelezo wake.