
WASHINDI wanne wa droo ndogo ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba awamu ya pili, inayoendeshwa na Global Publishers, leo wameangua vicheko vya furaha baada ya kupewa zawadi zao kama walivyoshinda katika hafla iliyofanyika ndani ya ofisi za kampuni hiyo, Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Walioshinda ni Victor Mubi wa Mwenge aliyejishindia zawadi kubwa ya pikipiki katika droo hiyo, ambaye alipewa zawadi yake na Mr. Shinda Nyumba, huku Josephine Bonifasi wa Songea aliyejishinda televisheni (flat screen), akiwakilishwa na Amina Mbunda ambaye alikabidhiwa zawadi yake na mwakilishi wa British School, Selestini Moshi.

Ramadhan Zuher wa Morogoro aliyeshinda zawadi ya simu ya kisasa aina ya smartphones, aliwakilishwa na Sufiani Kassim, ambaye zawadi yake alipewa na Halima Kaudasio, mwakilishi wa Ting, ambao ni wadhamini mwenza wa shindano hilo huku Rose Willbrad Mlay wa Kunduchi, aliyeshinda Dinnerset, alikabidhiwa zawadi yake na Mhariri wa gazeti la Ijumaa, Amrani Kaima ‘Kakitu’.

Hii ni droo ndogo ya pili iliyofanyika Machi 17 mwaka huu, katika viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala baada ya ile ya kwanza ya Februari 8, ambayo ilichezeshwa katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala.









Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Championi, Amani, Risasi, Ijumaa Wikienda na Uwazi, Abdallah Mrisho, ni mpango wa kampuni kuona kuwa droo ndogo zinachezwa kila mwezi na kwamba zawadi zitaboresha.
Na Mwandishi Wetu/GPL