×

Maumivu ya Kiuno, Mgogo-2

Na TABIBU WA UWAZI| GAZETI LA UWAZI| AFYA

AINA kuu za maumivu ya mgongo mara nyingi, maumivu ya mgongo hujitokeza katika aina kuu mbili ambayo ni maumivu yanayosambaa, maumivu yasiyohama  ambayo yapo katika eneo la mgongo ( localized pain).

Maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli au mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa na kitu kizito eneo la mgongoni na kuchana misuli yake. Au, ni yale yanayotokana na mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo. Yapo mamivu yanayosambaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili mbali na mgongo kama vile miguu.

Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo kwa kupigwa/kuanguka kwa mfano tatizo linakuwa  mgongoni ila unahisi ganzi kwenye mguu ambayo huwaka moto.

Visababishi vya maumivu ya mgongo ni kama vile kubeba mizigo mizito, kukaa au kusimama kwa muda mwingi nyumbani, kazini, shuleni, n.k wakati unafanya shughuli zako za kila siku, una nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza hatari ya kupata maumivu ya mgongo. Lakini pia kulalia godoro laini na lililobonyea katikati husababisha kuumwa kwa mgongo.

Hii husababisha misuli ya mgongo kuvutika kupita kiasi wakati umelala na kusababisha kuchanika misuli ya mgongo. Wengine hupata maumivu kwa kujeruhi mgongo kutokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe kama wa kansa katika uti wa mgongo.

Ujauzito na uzito wa kupita kiasi kama kuwa na kitambi husababisha maumivu ya mgongo, ila wajawazito wanafahamu wao hubadili mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimama hivyo kusababisha maumivu.

Msongo wa mawazo (stress) humfanya mtu kukaa katika mkao mbaya akiwaza hivyo kupata maumivu ya mgongo. Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo na misuli ya pembeni mwa mifupa pia husababisha maumivu katika eneo husika.

Kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake ya awali kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ajali na uzeeni, husababisha maumivu ya mgongo.